41
Tafsiri
No.14
Sheria ya Makosa ya Mtandao
2015
3. Katika Sheria hii, isipokuwa kama muktadha
utahitaji vinginevyo“kuingia” kuhusiana na mfumo wa kompyuta, maana yake ni
kuingia, kutoa maelekezo, kuwasiliana, kuhifadhi
data au kupokea data kutoka katika mfumo wa
kompyuta au vinginevyo kutumia nyenzo zozote za
mfumo wa kompyuta, mtandao au chombo cha
kuhifadhia data;
“mtoa njia” maana yake ni mtu anayetoa huduma ya
usambazaji wa data za kielekroniki kwa kusambaza
taarifa zilizotolewa na, au kwa mtumiaji wa huduma
katika mtandao wa mawasiliano au kutoa fursa ya
kuingia kwenye mtandao wa kompyuta;
“mhifadhi data ” maana yake ni mtu anayetoa huduma ya
uhifadhi wa data za kielektroniki kwa njia
inayojiendesha yenyewe, kwa kupitia mtu kati au
kwa utunzaji wa taarifa wa muda mfupi, kwa
madhumuni ya kuwezesha upatikanaji wa taarifa kwa
kwa watumiaji wengine wa huduma kiufanisi zaidi,
pale watakapoomba;
“mtoto” maana yake ni mtu mwenye umri chini ya miaka
kumi na nane;
“ponografia za watoto” maana yake ni aina ya picha na
filamu za ngono zinazoashiria au kumuonesha:
(a) mtoto akiwa anashiriki kwa uwazi matendo ya
ngono;
(b) mtu anayeonekana kama mtoto akiwa anashiriki
kwa uwazi matendo ya ngono; au
(c) taswira inayoashiria mtoto akiwa anashiriki kwa
uwazi matendo ya ngono;