Na.14
Sheria ya Makosa ya Mtandao
2015
42
“mfumo wa kompyuta” maana yake ni kifaa au
mchanganyiko wa vifaa, ikijumuisha mtandao, vifaa
vya kuingizia na vya kutolea na vinavyoweza
kutumika pamoja na majalada
ya nje yenye
programu za kompyuta, maelekezo ya kielektroniki,
data za kuingizia na kutolea zinazotunza data za
hesabu za miongo zilizo na mantiki, utunzaji wa data
za hesabu na udhibiti wa utolewaji wa mawasiliano
na majukumu mengine;
“data kompyuta” maana yake ni uwasilishaji wa maelezo,
dhana, taarifa au maelekezo katika namna inayofaa
kuchakata katika mfumo wa kompyuta,ikijumuisha
programu inayofaa kuuwezesha mfumo wa kompyuta
kutelekeza kazi fulani;
“chombo cha utunzaji wa data ” maana yake ni kifaa
chochote au kitu ambacho kwayo kompyuta au
taarifa inaweza kutunzwa au kutengenezwa ama kwa
msaada wa kifaa kingine au kitu au la;
“kifaa” inajumuisha:
(a) programu ya kompyuta, namba tambuzi au mianzi
laini;
(b) sehemu ya mfumo wa kompyuta kama vile grafiki
kadi, kadi ya kutunza kumbukumbu, chipu au
kichakataji;
(c) kifaa cha kutunzia kumbukumbu za kompyuta; na
(d) kifaa cha kuingizia na kutolea taarifa katika
kompyuta na mifumo ya kompyuta;
“mawasiliano ya kielektroniki” maana yake ni uhamishaji
wowote wa alama, ishara au data kompyuta ya aina
yoyote ile iliyotumwa yote au sehemu yake kwa njia
ya waya, redio, elektromagnetiki, picha ya
kielektroniki, picha ya